PROJECTS

IMMANUEL ORPHANAGE AND SOCIAL DEVELOPMENT

ENEO LA KITUO
Tunategemea kujenga kituo chetu chenye ukubwa wa zaida ya ekari 5. Kituo hicho kitakuwa na vyumba vya kulala, sehemu ya kulia chakula, sehemu ya mapumziko (eneo la wazi), ofisi, eneo la ufugaji na kilimo, eneo la michezo, dispensari, shule ya chekechea, na ya msingi, eneo kwaajili ya mafundisho mbalimbali, nyumba kwaajili ya wafanyakazi, eneo la sanaa

SHULE
Elimu tuanyotaka kuitoa kwa vijana wetu ni elimu ya chekechea na ya msingi. Shule yetu itakuwa ni shule ya "English Medium" ambapo wanafunza watajifunza sana jinsi ya kuongea lugha ya kingereza na pia kujifunza lugha Kiswahili. Lengo letu ni kutaka kuwaweka vijana katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.

KILIMO NA UFUGAJI
Tunampango wa kuanzisha kilimo na ufugaji kwaajili ya chakula kwa vijana watakaokuwepo katika kituo chetu. Kwa kuanza, tunataka kuanza na ufugaji wa kuku wa mayai na nyama na katika kilimo tunategemea kuanza na kilimo cha mbogamboga.

MATIBABU
kituo hiki kitakuwa na kituo cha afya kwaajili ya vijana watakaokuwa wanaishi mahali hapo. Vijana watatibiwa bure. Lengo letu ni kuwaweka vijana katika afya na kuishi maisha ya amani.

MICHEZO
Tunatakuwa na michezo mbalimbali kwaajili ya vijana. Baaadhi ya michezo tutakayokuwa nayo ni kama, mpira wa miguu (football), mpira wa mikono (netball na valleyball), tennis, mchezo wa kikapu (basketball), mchezo wa riadha, na michezo mingine mingi itayopendwa na vijana wetu. Kutakuwa na walimu wa kufundisha hiyo michezo.

Madhumuni yetu ni kutaka kujua vipaji vya vijana katika michezo, na kuwainua mpaka kufikia malengo yao. Pia kuwajenga vijana kuwa imara na shujaa.

VYUMBA VYA KULALA
Kutakuwa na vyumba vya kulala, ambapo kutakuwa na kitanda, meza ya kusomea na kabata dogo la kuweka vitabu, sehemu ya kuhifadhi nguo.

NYUMBA ZA WAFANYAKAZI
Wafanyakazi watakuwa na mahali pao pa kuishi, hawatachangamana na vijana. Wao watapewa nyumba na vifaa vya muhimu kwaajili ya kukidhi mahitaji yao

OFISI
Kutakuwa na ofisi za walimu wa chekechea, walimu wa shule ya msingi, walimu wa dini, walimu wa michezo. Kila ofisi itakuwa na meza, viti na kabati kwaajili ya kutunzia vitabu. Vifaa vya ufundishaji vya kisasa vitakuwepo.

 BIASHARA
Tunategemea kuanzisha biashara zetu zitakazojikita sana katika mazao ambayo tutakuwa tunazalishan katika kituo chetu. Baadhi ya biashara tutakazofanya ni kama uuzaji wa kuku za kisasana za kienyeji, uuzaji wa mayai, uuzaji wa sanaa zitakazotengenezwa na vijana wetu, uuzaji wa mboga za majani zinazozalishwa na vijana.

SANAA
Vijana wenye vipaji mbalimbali watajikita katika sanaa. lengo ni kuinua vipaji vyao kwa njia ya sanaa. Kama kutakuwa na mahitaji ya vifaa kwaajili ya sanaa, kituo kitaaanda vifaa hivyo.